local News

wanaume washauriwa kupima tezi dume

Wanaume mkoani TABORA wameshauriwa kupima mara kwa mara katika vituo vya afya ili kuepukana na tatizo la saratani ya tezi dume ambalo limekuwa tishio kwa sasa.

Ushauri huo umetolewa na Kaimu Mganga Mkuu wa kituo cha afya cha EPHATA, kilichopo mjini TABORA,Daktari JUSTINA MKOME wakati akizungumza na CG FM kuhusu tatizo la saratani ya tezi dume ambapo amesema tatizo hili ni hatari pale linapompata mwanaume hivyo ni vyema kuchukua tahadhari mapema.

Daktari MKONE ameongeza kuwa moja ya dalili za tatizo la saratani ya tezi dume ni kusikia maumivu wakati wa haja ndogo na kutokwa damu wakati wa haja ndogo.

Taarifa ya HASSAN KITUNGA.


Wakazi wa mkoa wa DODOMA wametakiwa kushiriki katika maadhimisho ya kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto wa kike

Wakazi wa mkoa wa DODOMA wametakiwa kushiriki katika maadhimisho ya kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto wa kike kwa lengo la kupunguza vitendo hivyo.

Akizungumza na wanahabari juu ya maadhimisho ya kupinga ukatili na unyanyasaji wa Kijinsia,Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa DODOMA, Kamishna Msaidizi wa polisi ERNEST KIMOLA amesema maadhimisho hayo yatafanyika kuanzia kesho hadi tarehe kumi mwezi ujao.

Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la kupinga ukatili wa kijinsia la AFNET, Bi SARA MWAGA amesema huduma mbalimbali za msaada wa kisheria zitatolewa ili jamii iweze kupata uelewa aina mbalimbali za ukatili unaofanyika kwenye baadhi ya maeneo.

Naye Profesa ADAM MWAKILOBO wa Chuo Kikuu cha DODOMA amesema maadhimisho hayo yawe chachu ya kuondoa dhana ya kuwanyanyasa watoto wa kike katika ukatili wa kijinsia na aina nyingine ya ukatili unaofanyika.

Taarifa ya PIUS JAYUNGA.


wananchi wa kata ya NDEVELWA katika halmashauri ya Manispaa ya TABORA kulima zao la alizeti ili kuondokana na umaskini.

Wananchi wa kata ya NDEVELWA katika halmashauri ya Manispaa ya TABORA wameanza kilimo cha alizeti ili kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini .

Diwani wa kata hiyo,Bwana SELEMAN MAGANGA ameeleza hayo wakati wa ziara ya mbunge wa jimbo la TABORA mjini,Mheshimiwa EMMANUEL MWAKASAKA alipotembelea mradi wa mashine ya kukamua mafuta ya alizeti unaoendeshwa na vikundi vya wajasiriamali katika kata hiyo.

Akisoma risala kwa niaba ya wanavikundi wa ufugaji na kilimo katika ya NDEVELWA,Bwana SEIF SALUM amesema wana imani watakamilisha ufungaji wa mashine kinu cha kukamua mafuta ya alizeti endapo watapata msaada wa shilingi milioni moja na nusu.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la TABORA mjini,Mheshimiwa EMMANUEL MWAKASAKA amesema ataendelea kushirikiana na wananchi wa jimbo lake katika kutatua changamoto kadri atakavyojaliwa.

Naye mkuu wa wilaya ya TABORA,Mwalimu QUEEN MLOZI ameeleza kuridhishwa na hatua iliyofikiwa na wananchi katika ujenzi wa mashine ya kukamua mafuta ya alizeti.

Amesema wananchi wa mkoa wa SINGIDA wameinuka kiuchumi kutokana na kilimo cha alizeti hivyo wananchi wa TABORA nao waige mfano wa wananchi wa SINGIDA.

Taarifa ya VIVIAN PYUZA.

our programs

Sikiliza kuanzia Jumatatu-Ijumaa 1:00pm-2:00pm and 06:00pm-06:30pm
Jumatatu-Alhamisi 11:02pm - 13:00pm
Sikiliza kila siku ya wiki kuanzia saa 07:30am hadi 08:00am
Sikiliza kila siku ya wiki kuanzia saa 08:00am hadi 08:02am
sikiliza kuanzia saa 08:02am hadi 11:00am jumatatu - Alhamisi