News


Idadi ya wanafunzi wanaotarajia kufanya mtihani wa darasa la saba

Idadi ya wanafunzi wanaotarajia kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu imeongezeka kutoka 4313 mwaka jana, hadi wanafunzi 4444 wakiwemo wavulana 2110 na wasichana 2334, Toa maoni yako katika taarifa yetu ya habari ya nusu saa kuanzia saa kumi kamili alasiri, kupitia 89.5 CG FM RADIO-TABORA.


Papa Francis amtawaza Mama Teresa kuwa mtakatifu

Maelfu ya watu wameshuhudia ibada ya kutawazwa kuwa mtakatifu, ambapo Papa Francis amemtangaza mtawa Mama Teresa kuwa mtakatifu.

Raia huyo wa Albania ambaye alifariki mwaka wa 1997 alianzisha shirika la hisani la kimishenari ili kuwasaidia walala hoi katika mtaa wa mabanda wa Calcutta nchini India.

Atajulikana kuwa mtakatifu Teresa wa Calcutta. Waandishi wnasema kuwa maisha yake yanaenda sambamba na maono ya Papa Francis kuhusu kanisa linalojikakamua kuwasaidai watu masikini.

Lakini wakosoaji wanasema kuwa Mama Teresa hakuwasaidia watu waliokuwa wagonjwa ,na alilaumiwa kwa kujaribu kuwabadilisha dini watu masikini wa kabila la Hindu nchini India kuwa Wakristo.


Ijue TABORA

Mji ulianzishwa katika nusu ya kwanza ya karne ya 19 na wafanyabiashara Waarabu na Waswahili kutoka Zanzibar. Waliitumia kama kituo kwenye njia ya biashara kati ya pwani na Ziwa Tanganyika. Biashara kuu ilikuwa ndovu pamoja na watumwa. Tabora walijenga nyumba imara pamoja na ghala za bidhaa kwa ajili ya biashara hii. Familia ya Tippu Tip ilikuwa kati ya wenye nyumba wa Tabora. Mwaka 1871 jeshi la rugaruga wa Mtemi Mirambo ilishambulia mji. Ukajengwa upya. Tangu 1890 Wajerumani walianza kufika na baada ya kushinda Wanyamwezi walifanya Tabora kuwa kitovu chao katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ya kati; mji ukawa kituo cha kikosi cha jeshi na pia kikosi cha polisi. Umuhimu wa Tabora ikaongezeka kwa ujenzi wa reli ya kati iliyounganisha pwani na Ziwa Tanganyika ikipita Tabora na karahana muhimu ya reli ikawekwa hapa mjini. 1916 Tabora ilivamiwa na Wabelgiji waliowafukuza Wajerumani lakini baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia mji ukawa sehemu ya Tanganyika. read more


Malkia wa Taarab Bi Shakila aliyefariki Aug 19

Shakila Said Hamis… Jina lake lina uzito mkubwa sana kwenye muziki wa Taarab anafahamika kama miongoni mwa wasanii waliotamba miaka kadhaa na hits single ikiwemo Kifo cha mahaba, Mapenzi yamepungua na nyinginezo. Read more


Application iliyozinduliwa kwa ajili ya kuzuia ajali barabarani

Polisi nchini kwa kushirikiana na kampuni ya Makini Road Safety Foundatini imeturahisishia njia nyepesi ya kukabiliana na ajali za barabarani ambapo kwa kutumia application ya MakiniApp ambayo ukiwa nayo katika simu yako inakusaidia kujua mwendokasi wa dereva kwenye gari ulilopanda. read more


Dodoma yatajwa kuwa kinara wa viashiria vya ugonjwa huu

Mkoa wa Dodoma umetajwa kuwa na viashiria vya juu katika maambukizi ya UKIMWI ikilinganishwa na mikoa mingine. Hali hiyo imetokana na kuwepo kwa vitu kadhaa vinavyowakutanisha vijana vikiwamo vyuo na sehemu za starehe.
Akizungumza na Gazeti la Mtzanzania, mratibu wa programu za kanda za Afrika, Renatus Kihongo alisema utafiti uliofanywa mwaka 2012 unaonesha vijana wengi katika manispaa ya Dodoma wanatumia muda mwingi kwenye starehe jambo ambalo ni linatishia uwepo wa maambukizi ya ugonjwa huo.
Utafiti huo ulifanywa na Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania ‘TACAIDS’ viashiria vya maambukizi ya UKIMWI vipo juu kwa vijana kati ya miaka 15 hadi 24 ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu ndio wanaonekana kuwepo katika viashiria hivyo. read more

our programs

Sikiliza kila siku ya wiki kuanzia saa 06:00 hadi 06:30
Sikiliza kila siku ya wiki kuanzia saa 06:30 hadi 07:00
Sikiliza kila siku ya wiki kuanzia saa 07:30 hadi 08:00
Sikiliza kila siku ya wiki kuanzia saa 08:00 hadi 08:02
kuanzia saa 08:02 hadi 11:00