sports newsMILAMBO FC ya TABORA yatoa mapumziko ya wiki mbili kwa wachezaji wake

Uongozi wa timu ya MILAMBO FC ya TABORA umetoa mapumziko ya wiki mbili kwa wachezaji wake kufuatia kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa michuano ya ligi daraja la pili TANZANIA BARA.

Katibu Msaidizi wa timu hiyo MRISHO KAPAJA amesema baada ya mapumziko hayo kumalizika timu itajiandaa na mzunguko wa pili kadhalika maandalizi kwa ajili ya michuano ya kombe la FA nchini.

MILAMBO imemalizika mzunguko wa kwanza ikiwa na alama tano kwa michezo MINNE ikishinda moja kutoka sare mara mbili na kupoteza mchezo moja.

Taarifa imeandaliwa na ADAM HHANDO.


Wananchi wa mkoa wa TABORA wametakiwa kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika kongamano la michezo mbalimbali linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni mkoani hapa.

Wananchi wa mkoa wa TABORA wametakiwa kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika kongamano la michezo mbalimbali linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni mkoani hapa.

Akizungumza na CG FM mkuu wa wilaya ya TABORA.Mwalimu QUEEN MLOZI amesema kongamano hilo lina lengo la kuwakumbusha wananchi mkoani TABORA umuhimu wa kufanya mazoezi.

Ameongeza kuwa kongamano hilo litahusisha michezo mbali mbali pamoja na vikundi vya sanaa kutoka mkoani TABORA. Kongamano hilo litafanyika Jumapili ya wiki hii katika viwanja vya Chuo cha Utumishi wa Umma-UHAZILI

Taarifa imeandaliwa na ADAM HHANDO.


ANDY MURRAY atwaa tuzo ya kwanza fainali za Dunia za ATP 2016

Mcheza Tennis MWINGEREZA ANDY MURRAY amefanikiwa kunyakua tuzo ya kwanza fainali za Dunia za ATP 2016 kufuatia kumshinda NOVAK DYOKOVICHI MURRAY mwenye miaka 29 ameshinda fainali hizo kwa ushindi wa 6-3 6-4 katika uwanja wa O2 arena mjini LONDON.

Baada ya ushindi huo mshindi huyo amesema ana furaha kubwa sana kuwa mshindi, na kuwa namba moja duniani ni kitu cha kipekee sana akizingatia ameshinda NOVAK katika mashindano kama hayo.

Taarifa imeandaliwa na ADAM HHANDO.

our programs

Sikiliza kuanzia 4:15pm - 6:30pm FRIDAY
Sikiliza kila siku ya wiki kuanzia saa 06:30am hadi 07:00am
Sikiliza kila siku ya wiki kuanzia saa 07:30am hadi 08:00am
Sikiliza kila siku ya wiki kuanzia saa 08:00am hadi 08:02am
kuanzia saa 14:00pm - 16:00pm jtatu - Alhamisi