EnterntaimentCOLLABO YA DAVIDO NA TINASHE YAFANA.

Staa wa hit singles kutoka West Africa, Nigeria Davido ameachia nyimbo mpya yake mpya aliyomshirikisha mwimbaji Mmarekani mwenye asili ya Zimbabwe Tinashe wimbo huo unaitwa “How Long”.

Nyimbo hio imeachiwa siku ya Alhamis tarehe 13 Mwezi huu na mpaka sasa video hio imefikisha 788,603 kwa kuangaliwa kwenye mtandao.

Wimbo huo wenye mahadhi ya kiafrika umetayarishwa na Mtayarishaji wa Mziki Spellz ,Kumbuka Davido ni mmoja kati ya wale wasanii waliopata mkataba na Kampuni kubwa ya Sony Music Entertainment International Limited iliyo na makao Makuu yake South Afika.

By Najjat Omar.


LILY WAYNE, BIRDMAN SIO MWANA FAMILIA KWANGU

Uhasama kati ya Lily wayne na Birdman bado una ufa mkubwa sana baada ya Lil Wayne kusema kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Cash Money Birdman kuwa sio mwanafamila kwake.

Uhasama huo unachukua sura mpaka kila siku na mpaka sasa hakuna ishara yoyote inayoonesha ishara ya wawili hao kupatana hivi karibuni.

Lily wayne alihojiwa hivi karibu kwenye na mtandao HipHollywood, Wayne alipoulizwa kuhusu jinsi uhusiano wake na baba yake (akimaisha Birdman aliyewahi kumsimamia kwa miaka 20 kwenye kazi za mziki) majibu yake yalikuwa hayana matumaini ya kupatana na Birdman.

"Mimi nina umri wa miaka 34 na mtoto pia, Mimi ni mzee “aliendelea kuzungumza bila kuficha. "Jina langu la mwisho halihusiani na ubini ,Yeye si familia, "Wayne alimaliza.

Lil Wayne kwa sasa yupo katika ziara ya kusafiri katika nchi yote ya Marekani ili kukuza kitabu chake kipya cha Gone 'Til November .

By Najjat Omar.


ZAYN MALIK KUWA DESIGNER VERSUS VERSACE

Kampuni ya Versace ya usambazaji wa nguo imebaini kua uambaji wa Zayn Malik ni mkubwa na kuamua kumchukua kama designer mpya, ahadi hiyo ilitolewa na Makamu wa Rais wa Versace Donatella Versace. "Versus ni roho ya familia Versace na daima imekuwa ikishirikiana na muziki,Kila mtu kutoka Foo Fighters na Lenny Kravitz amekuwa katika maonyesho, na wote wanafaa , Kwangu mimi, Zayn alikuwa anafaa na amekamilifu. " alisema Bi Versace. Alisema kuwa Zayn Malik ni msanii mwenye heshima na anafaa sana kuwa kwenye Kampuni hio,alimtafuta siku nyingi ila ratiba zao zilikuwa haziko sawa. Wasanii wengi maarufu ni wanamitindo wa Mavazi hayo ya VERSUS VERSACE.

By Najjat Omar.


LAKTI YA DHAHABU YA TUPAC SHAKUR KUUZWA.

Lakti hio ambayo ilikuwa kwenye cheni ya Tupac wakati anashambuliwa kwa risasi mwaka 1994 inaiuzwa kwa gharama ya $ 125k.

Muuzaji wa vitu vya kumbukumbu wa, Moments In Time, amesema kuwa lakti hio inaunzwa kwa kiasi hicho cha fedha kwa haraka na ,lakti hio imepinda kutokana na risasi ambazo zilipita kwenye mwili wa Tupac

Gary Zimet amesema kuwa lakti hio ilikuwa ikivaliwa kwenye cheni na marehemu Tupac,na wakati mabako anashambuliwa alikuwa nayo shingoni, Familia ya Tupac imeamua kuuza ili waweze kupata faida kubwa.

Kwa mujibu wa Mwanasheria wa Tupac amesema kuwa hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuuza bidhaa yoyote Tupac, hata familia pia, Imeeleza kuwa atayefanya hivyo atalipa faini na yoyote atayenunua atalipa faini pia.

By Najjat Omar.


BINTI WA MWANARIADHA WA MAREKANI TYSON GAY AUAWA

Binti wa mwanariadha wa Marekani na mshindi wa Olimpiki, Tyson Gay mwenye umri wa miaka 15 ameuawa kwa kupigwa risasi alipokuwa kwenye mgahawa huko Kentucky.

Binti huyo Trinity Gay, ambaye tayari alikuwa ameanza kuwa maarufu, amepigwa risasi ya shingoni siku ya tarehe 16 Octoba mwaka huu, Alipelekwa hospitali papo hapo naalipofika hospitali kufariki kutokana na kumwagika kwa dau nyingi.

Baba yake amesema kuwa amechanganyikiwa na hajui nini kimetokea kwa sasa alikuwa kwake wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa polisi waliokuwa hapo wamesema kuwa kulikuwa na majibizano ya risasi kati ya gari mbili, Trinity, hakuwepo kwenye gari lolote kati ya hayo ambayo yalikuwa yanarushiana risasi inawezakana ikawa ni mpita njia tu.

Trinity alikuwa amefuata nyayo za baa yake kwa kukimbia mbio za mita 100 na 200 shuleni.

By Najjat Omar.


MJUKUU WA KIBAKI AACHANA NA MPENZI WAKE.

Andrew Sean Kibaki, ambaye ni mjukuu wa Rais Mstaafu wa Kenya amegonga vichwa vya habari kwa kuachana na aliyekuwa mpenzi wake nyota wa mtandao wa YouTube Elodie Zone,Taarifa za kuachana kwao zilipata kwenye mazishi ya bibi yake Lucy Kibaki.

Elodie ameandika '' Mimi rasmi nimeamua kukaa mbali na mahusiano na Sean”

Ameongezea kwa kusema kuwa umefika mda sahihi sasa wa yeye kujenga himaya yangu mwenyewe na na kuwa huru na maisha yangu binafsi, Anaendlea kusema kuwa Sean alikuwa na msaada mkubwa kwenye maisha yake na hakuna mahusiano ya milele cha muhimu ni kuwa kawaida na sio kuweka ugomvi.

Mahusiano ya Sean na Elodiea yalianza mwaka 2015 na kuvunjika mwaka 2016 mwezi Octoba ,huku Elodie akiwa anaendelea na maisha yake ya kawaida ikiwa mpaka sasa sababu ya kuachana kwao haijajulikana.

By Najjat Omar.

our programs

Sikiliza kila siku ya wiki kuanzia saa 06:00am hadi 06:30am
Sikiliza kila siku ya wiki kuanzia saa 06:30am hadi 07:00am
Sikiliza kila siku ya wiki kuanzia saa 07:30am hadi 08:00am
Sikiliza kuanzia 2:00pm - 4:00pm jtatu hadi Alhamisi
kuanzia saa 2:00pm - 4:00pm FRIDAY only